📘 قراءة كتاب SIFA ZA MKE MWEMA أونلاين
Utangulizi................................................................................................................................. 3
Kanuni ya sifa za mke mwema ............................................................................................. 5
Mke mwema uhusiano wake na Allaah............................................................................... 7
Mke mwema uhusiano wake na Shetani ........................................................................... 12
Mke mwema anatakiwa kumfurahisha mume................................................................. 14
Mke mwema anatakiwa kumtii mume .............................................................................. 17
Mke mwema anatakiwa kutofanya upungufu katika haki za mume ........................... 21
Mke mwema hamtii mume wake uzito katika matumizi ............................................... 22
Mke mwema hatakiwi kukufuru neema kwa mume wake ............................................ 24
Mke mwema anatakiwa kumheshimu mume wake........................................................ 25
Mke mwema anatakiwa kuwa muadilifu kwa watoto wake ......................................... 27
Mke mwema anatakiwa kubaki nyumbani....................................................................... 28
Mke mwema hatoi siri za mume wake .............................................................................. 29
Hitimisho................................................................................................................................ 30
Himidi zote ni Zake Allaah. Tunamhimidi na kumtaka msaada na kumuomba
mswamaha na tunatubu Kwake. Tunajikinga kwake kutokana na shari ya nafsi
zetu na matendo yetu maovu. Mwenye Kuongozwa na Allaah hakuna wa
kumpoteza. Mwenye Kupotezwa na Allaah hakuna wa kumwongoza.
Nashuhudia ya kwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki
isipokuwa Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika. Nashuhudia ya kwamba
Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, Swalah na salaam zimwendee yeye,
ahli zake na Maswahabaha zake wote.
Amma ba ́ad...
Maudhui ya Risaalah hii iliyo na anuani ”Sifa za mke mwema” hayamuhusu tu
msichana mdogo ambaye yuko katika njia ya kutaka kuolewa na anataka kujua
sifa ambazo mke anatakiwa kuwa nazo ili ajiandae nazo, kuishi nazo na
kuzitimiza.
Vilevile hayamuhusu tu mwanamke ambaye ameolewa ambaye anataka kuwa na
sifa za mke mwema ili aweze kuzidhibiti na kuishi nazo katika maisha yake.
Vilevile hayamuhusu tu mwanamke mwenye upungufu ili aweze kutibu
upungufu wake na kujisahihisha mwenyewe na ndoa yake tukufu.
Ni wito na ukumbusho ulio jumla kuliko hivyo.
Ni ukumbusho kwa baba ambaye anataka wasichana zake na wanawake ambao
wako katika usimamizi wake wapate kukuwa vizuri na malezi mazuri na ndoa
ambayo inaafikiana na Matakwa ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam). Kwa
kupitia kalima hii itakuwa ni usaidizi kwake kuweza kuwakumbusha vidhibiti
vya Shari ́ah na sifa ambazo inatakikana kwa msichana kukuwa juu yake.
Kadhalika ni ukumbusho kwa mama ambaye ni mchungaji katika nyumba yake
na wasichana wake na kuwatengeneza. Wasichana wengi wanakuwa kwa tabia
na sifa mbalimbali ambazo wamepata kutoka kwa wamama zao.
Sifa Za Mke Mwema
Shaykh ́Abdur-Razzaaq bin ́Abdil-Muhsin
Kadhalika ni ukumbusho kwa walinganiaji ili waweze kuliwekea uzito hili,
kutiliia umuhimu na kufanya juhudi katika kueneza sifa hizi tukufu, tabia
zilizosifiwa na kazi iliyobarikiwa ili ziweze kupatikana kwa wasichana na
wanawake katika jamii ya imani na majumbani. Hili ni khaswa hivi leo wakati
mwanamke ameshambuliwa kwa njia ambayo kamwe haijawahi kuonekana
hapo kabla. Inafanyika kwa kutumia namna na njia mbalimbali. Malengo ni
kutaka kumpotezea mwanamke heshima yake, utukufu wake, ukamilifu wake,
fadhila zake, uzuri wake, imani yake, tabia yake na wema wake.
Hapo kabla ilikuwa ni vigumu sana kwa mwanamke kufikiwa na propaganda
zinazoharibu, matamanio ya udanganyifu na maoni yaliyofungamana. Hilo
lilikuwa likitendeka ima kwa kupitia rafiki mbaya au mfano wa hayo. Ama leo
mwanamke anafikiwa na uchafu na uharibifu wote wa duniani nyumbani kwake.
Hahitaji kutoka nje kwa ajili ya hilo. Sasa mwanamke anaweza kukaa chumbani
mwake mbele ya TV, intaneti au magazeti machafu na akapata uchafu na shari
zote katika moyo wake na fikra zake. Ili aweze kuwa mwema, mtwaharifu,
mwenye Dini na mwenye kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta ́ala) analazimika kufunga
madirisha, njia na mwanya wa kila shari na uharibifu.
Mwanamke ana majukumu makubwa kwa wale watu ambao anawasimamia.
Suala hili linahitajia kuliwekea umuhimi mkubwa kabisa.
Katika kivuli cha hali hii na upungufu wa ukumbusho na ukumbusho wa imani,
tabia nzuri na maelezo mazuri ambayo mwanamke anatakiwa kuwa nayo,
wanawake wengi wamekuwa wadhaifu. Wametumbukia katika kuwa na
upungufu katika haya na Dini na kuanguka katika upungufu mwingi na
kuathirika.
Kalima hii ni kama tulivyosema ni kuhusu sifa za mke mwema. Ninamuomba
Allaah Mtukufu, Mola wa ́Arshi kubwa, afanye iwe ya kheri na manufaa na
afanye iwe ni ufunguo wa kheri ufunge shari na uongoze nyoyo, uzitengeneze
nafsi na ufanye kuwepo mawasiliano na Mola wa walimwengu ili Radhi Zake na
Mapenzi Yake viwezi kufikiwa na kuepuka yale yanayomkasirikisha na
kumghadhibikisha (Jalla wa ́Alaa).
Wakati tunapozungumzia kuhusu sifa za mke mwema na wema hatutakiwi
kupuuza kanuni kubwa ambayo ni kanuni ya msingi ya kufikia wema, nayo ni
kwamba wema hauwezi kufikiwa isipokuwa kwa mambo mawili:
Jambo la kwanza ni uafikishaji wa Allaah (Jalla wa ́Alaa), uongofu Wake, msaada Wake,
usahali Wake na uafikishaji. Mwenye Kuongoza ni Allaah. Ndiye Muwafikishaji.
Mambo yote yako Mikononi Mwake (Jalla wa ́Alaa). Allaah (Ta ́ala) Kasema:
Kitabu hii kinazunguzia sifa za mke mwema na namna ya kuzipata sifa hizo.
حجم الكتاب عند التحميل : 574.3 كيلوبايت .
نوع الكتاب : pdf.
عداد القراءة:
اذا اعجبك الكتاب فضلاً اضغط على أعجبني و يمكنك تحميله من هنا:
شكرًا لمساهمتكم
شكراً لمساهمتكم معنا في الإرتقاء بمستوى المكتبة ، يمكنكم االتبليغ عن اخطاء او سوء اختيار للكتب وتصنيفها ومحتواها ، أو كتاب يُمنع نشره ، او محمي بحقوق طبع ونشر ، فضلاً قم بالتبليغ عن الكتاب المُخالف:
قبل تحميل الكتاب ..
يجب ان يتوفر لديكم برنامج تشغيل وقراءة ملفات pdf
يمكن تحميلة من هنا 'http://get.adobe.com/reader/'