📘 قراءة كتاب HIJABU أونلاين
wajibu kwa mwanamke kuufunika uso wake mbele ya wanaume ajinabi............................... 4
2. Kufunika uso kunachangia kuhifadhi tupu................................................................................... 6
3. Uzuri wa mwanamke uko usoni..................................................................................................... 8
4. Uso ni mapambo yasiyotakikana kuonekana................................................................................ 9
5. Fitina iko usoni kwa mwanamke ..................................................................................................10
6. Uso wa mwanamke ni wenye fitina zaidi kuliko sauti ya mnyororo wake.................................. 11
7. Tofauti ya mwanaume mtu mzima na kijana ...............................................................................12
8. Wanawake bora zaidi walikuwa wakijifunika nyuso zao.............................................................14
9. Ni wajibu kwa mwanamke ajifunike mbele ya wanaume ajinabi................................................16
10. Cha kwanza mchumbiaji huangalia huwa ni uso .......................................................................16
11. Haijuzu kwa mwanamke kutoka kwenda mahala pa kuswalia bila ya mavazi ya juu ...............18
12. Wanawake wa kwanza walikuwa wakijifunika wanapotoka majumbani ..................................19
13. Ni wajibu kwa mwanamke kufunika miguu yake anapotoka nyumbani...................................21
14. Mwanamke anaruhusiwa kuonesha uso mtumwa wake........................................................... 22
15. Wajibu tu ndio iwezayo kuitikisa wajibu nyingine.................................................................... 23
16. Mwanamke kuonesha uso wake kuna madhara zaidi kuliko manufaa .................................... 25
17. Mwanamke kuonesha uso wake kunepelekea katika fitina....................................................... 26
18. Mwanamke kuonesha uso wake kunamwondosha haya........................................................... 27
19. Mwanamke kuonesha uso kunamfitinisha mwanaume............................................................ 28
20. Mwanamke kuonesha uso wake kunapelekea katika mchanganyiko ...................................... 29
21. Dalili juu ya kwamba inajuzu kwa mwanamke kuonesha uso.................................................. 32
22. Dalili za kujifunika ni zenye kutangulizwa juu ya dalili za kujifunua ...................................... 35
23. Tafsiri ya maneno ya Ibn ́Abbaas ............................................................................................ 36
al-Hijaab
Ibn ́Uthaymiyn
3
www.firqatunnajia.com
24. Tafsiri ya Hadiyth ya Asmaa ́.................................................................................................... 38
25. Tafsiri ya Hadiyth ya al-Fadhwl ................................................................................................ 39
26. Tafsiri ya Hadiyth ya mwanamke mwenye mashavu ya kupauka............................................40
27. Khitimisho ya kitabu "al-Hijaab"................................................................................................41
Himdi zote ni za Allaah. Tunamhimidi na kumuomba msaada na msamaha.
Tunajikinga Kwake kutokana na shari ya nafsi zetu na matendo yetu maovu. Yule
mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna awezae kumpoteza, na yule mwenye
kupotezwa na Allaah, basi hakuna awezae kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba
hapana mola wa haki isipokuwa Allaah na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni
mja na Mtume Wake. Allaah amswalie yeye, kizazi chake, Maswahabah zake na kila
mwenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
Amma ba ́d:
Allaah (Ta ́ala) amemtuma Muhammad (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam) na uongofu na dini ya haki
ili kuwaondosha watu kutoka gizani na kuwaongoza katika nuru, kwa idhini ya
Mola wao, kwenda katika njia [inayoelekeza kwa], Mwenye nguvu na msifiwa.
Allaah amemtuma ili aweze kuabudiwa Yeye mwenyewe kwa kukamilisha
udhalilikaji na unyenyekevu Kwake Allaah (Tabaaraka wa Ta ́ala) kwa kutekeleza maamrisho
Yake na kujiepusha na makatazo Yake na kutanguliza hayo mbele ya matamanio na
shahawa za nafsi. Allaah amemtuma vilevile ili kutimiza tabia njema na kulingania
kwayo kwa kutumia kila njia na kubomoa tabia zote mbaya na kutahadharisha nazo
kwa kutumia kila njia. Kwa ajili hiyo ndio maana Shari ́ah yake (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam)
imekamilika kwa njia zote. Haihitajii kiumbe mwenye kuikamilisha na kuipanga. Ni
yenye kutoka kwa mwingi wa hekima na Mjuzi wa yale yote ambayo ni mema kwa
waja Wake na ni Mwenye kuwahurumia.
Mfano mmoja wa tabia hizo nzuri alizotumwa nazo Muhammad (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam) ni
haya ambayo Mtume (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam) ameifanya kuwa ni sehemu katika imani.
al-Hijaab
Ibn ́Uthaymiyn
Hakuna yeyote mwenye kupinga ya kwamba Shari ́ah na desturi vyote viwili
vimemwamrisha mwanamke kuwa na haya na kuwa na tabia nzuri yenye kumkinga
na kutumbukia kwenye fitina na hali zenye utata. Ni jambo lisilokuwa na shaka
yoyote kwamba katika aina kubwa za kuwa na haya na kujiheshimisha ni pamoja na
yeye kujisitiri ikiwa ni pamoja vilevile na kufunika uso wake kwa kuwa
limnamlinda na kumkinga na kutumbukia kwenye fitina.
Hapo kabla watu katika mji huu uliobarikiwa - mji wa Wahyiy, ujumbe, haya na
heshima - walikuwa ni wazuri katika suala hili. Wanawake walikuwa wakitoka
wakiwa na Jilbaab, mbali kabisa na wanaume. Hali bado ni yenye kuendelea hivo
katika miji mingi ya kifalme na himdi zote ni Zake Allaah. Lakini pale baadhi ya
watu walipozungumzia juu ya Hijaab, kuwatazama wale wasiofanya hivo na
kuonelea kuwa ni sawa kwa mwanamke kuonesha uso, ndipo baadhi ya watu
wakaanza kutilia shaka Hijaab na kama ni wajibu kufunika uso au imependekezwa.
Au ni jambo tu ambalo ni la kimila na kidesturi na sio wajibu wala
haikupendekezwa?
Ili kuondoa shaka hii na kubainisha uhakika wa mambo ndipo nikapendelea
kuandika yenye kuweka wazi hukumu kwa kutaraji ya kwamba Allaah (Ta ́ala)
ataifanya iweke haki wazi na kutufanya sisi ni wenye kuongoka na kuiona haki na
kuifuata na batili na kuiepuka. Hivyo basi, ninamuomba Allaah mafanikio na
kusema:
Enyi waislamu! Tambueni ya kwamba mwanamke kujisitiri na kuufunika uso wake
mbele ya wanaume ajinabi ni jambo la wajibu. Uwajibu wake unatolewa dalili na
Kitabu cha Mola Wako (Ta ́ala), Sunnah za Mtume Wako (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam) na mtazamo
sahihi.
Kitabu hii kinazunguzia hijabu ya muislam sifa zake na hukumu zake.
حجم الكتاب عند التحميل : 804 كيلوبايت .
نوع الكتاب : pdf.
عداد القراءة:
اذا اعجبك الكتاب فضلاً اضغط على أعجبني و يمكنك تحميله من هنا:
شكرًا لمساهمتكم
شكراً لمساهمتكم معنا في الإرتقاء بمستوى المكتبة ، يمكنكم االتبليغ عن اخطاء او سوء اختيار للكتب وتصنيفها ومحتواها ، أو كتاب يُمنع نشره ، او محمي بحقوق طبع ونشر ، فضلاً قم بالتبليغ عن الكتاب المُخالف:
قبل تحميل الكتاب ..
يجب ان يتوفر لديكم برنامج تشغيل وقراءة ملفات pdf
يمكن تحميلة من هنا 'http://get.adobe.com/reader/'