📘 قراءة كتاب RIBAA أونلاين
Mada ya muhadhara ni kama mlivyosikia, ribaa na biashara za haramu au
zilizokatazwa. Ni mada ndefu ila tutajaribu kuifupisha na huenda
tukaikamilisha siku nyingine. Kwa kuwa watu wana haja kubwa ya mada
kama hii. Ribaa, Allaah Katoa makemeo makali sana katika kitabu Chake
Kitukufu. Kasema Allaah (Ta’ala):
“Wale walao ribaa hawasimami ila kama anavyosimama aliyezugwa na
shaytwaan kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: “Biashara ni kama
ribaa. Lakini Allaah Ameihalalisha biashara na Ameiharimisha ribaa. Basi
aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola Wake, kisha akajizuia, basi yake ni
yaliyokwisha pita, na mambo yake yako kwa Allaah. Na wenye kurudia basi
hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.” [Al-Baqarah 02: 275].
“Allaah Huiondolea baraka ribaa, na huzibariki swadaqah. Na Allaah
Hampendi kila [kaffar] mwenye kukanya na afanyae dhambi. Hakika wale
walioamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalah na wakatoa
Zaakah, wao watapata ujira wao kwa Mola Wao, wala haitakuwa khofu juu
yao, wala hawatohuzunika.” [Al-Baqarah 02: 276-277].
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni ribaa zilizobakia, ikiwa nyinyi ni
Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita Allaah na Mtume Wake. Na
mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.”
[Al-Baqarah 02: 278-279].
“Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na
mkiifanya deni kuwa ni swadaqah, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” [Al-
Baqarah 02: 280].
“Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa
ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.” [Al-Baqarah 02: 281].
Hizi Aayah ni za mwisho zilizoteremka katika Qur-aan kwa Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ’alayhi wa sallam). Na zimebeba maudhui ya ribaa, na
zimeweka wazi makemeo makali kwa walao ribaa. Jambo la kwanza
Katukhabarisha Allaah kuwa wale walao ribaa hawasimami ila kama
anavyosimama aliyezugwa na Shaytwaan kwa kumgusa. [Al-Baqarah 02: 275]
Nako ni wakati Allaah Atapowafufua watu katika hesabu watatoka katika
makaburi yao hali yakuwa wanatembea mbiombio. Hakuna yeyote
atakayeikwepa siku hii.
“Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia
mfundo, Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku
waliyokuwa wakiahidiwa.” [Al-Ma’aarij 70: 43-44].
“Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige waliotawanyika,
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.” [Al-
Qamar 54: 07-08].
Watatoka watu kwenye makaburi yao kwa idhini ya Allaah (Ta’ala) Ambaye
Amewapa uhai baada ya kuwa Amewafisha, na baada ya kuwa walikuwa
wamekwishasagika mifupa na nyama zao. Allaah Atawarudishia umbile lao
kama walivyokuwa mwanzo.
“Kama tulivyoanza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu
yetu. Hakika Sisi ni watendao.” [Al-Anbiyaa 21: 104].
Atatoka mtu kwenye kaburi lake na kuelekea katika upande Atapomuelekeza
- katika hesabu, hakuna yeyote atayekwepa. Watakuwa wakitembea mbio
mbio. Isipokuwa tu walao ribaa. Wao watatoka kwenye makaburi yao pamoja
na wengine, lakini watakuwa na fedheha kubwa. Watatoka kwenye makaburi
yao na watataka kutembea (kwenda) na wengine, wataanguka. Kila
wanapojaribu kusimama wanaanguka kama hali ya mwendawazimu ambaye
kashikwa na jini. Hivyo ni kwa sababu ribaa waliokula duniani bado imo
matumboni mwao. Wakijaribu kusimama na kutembea hawatoweza. Na hii
itakuwa fedheha na aibu kubwa kwao mbele ya watu. Hali haitoishia hapo.
Bali Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Kawapa makemeo mbalimbali. Anasema
Allaah:
“Basi aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola Wake, kisha akajizuia.” [Al-
Baqarah 02: 275].
Yaani atakayetubu kwa [kula] ribaa baada ya kujua uharamu wake.
“Basi yake ni yaliyokwishapita.” [Al-Baqarah 02: 275].
Allaah Husamehe yaliyopita kwake katika aliyoyafanya kabla ya kufanya
tawbah. Kama madhambi mengine, akitubia mtu kwayo hata kama ni
makubwa - hata kama ni shirki na kufru - atakayetubia tawbah ya kweli
Allaah
Humsamehe na humfutia dhambi zake.
Kitabu hii kinazunguzia riba na uharam wake
حجم الكتاب عند التحميل : 134.8 كيلوبايت .
نوع الكتاب : pdf.
عداد القراءة:
اذا اعجبك الكتاب فضلاً اضغط على أعجبني و يمكنك تحميله من هنا:
شكرًا لمساهمتكم
شكراً لمساهمتكم معنا في الإرتقاء بمستوى المكتبة ، يمكنكم االتبليغ عن اخطاء او سوء اختيار للكتب وتصنيفها ومحتواها ، أو كتاب يُمنع نشره ، او محمي بحقوق طبع ونشر ، فضلاً قم بالتبليغ عن الكتاب المُخالف:
قبل تحميل الكتاب ..
يجب ان يتوفر لديكم برنامج تشغيل وقراءة ملفات pdf
يمكن تحميلة من هنا 'http://get.adobe.com/reader/'