📘 قراءة كتاب TAFSIRI YA SHEMU YA KUMI YA MWISHO YA QUR rsquo ANI TUKUFU أونلاين
1
1.
FADHILA ZA QUR’ANI
2.
TAFSIRI YA SEHEMU YA KUMI YA MWISHO YA QUR’ANI
3.
MASWALI MUHIMU KATIKA MAISHA YA
MWISLAMU
4.
NI YAPI MAJINA MAZURI YA MWENYEZI MUNGU?
MATENDO YA NYOYO
6.
MAHOJIANO TULIVU
7.
KUKIRI KUWA HAKUNA ANAYE STAHIKI
KUABUDIWA ISIPOKUWA MWENYEZI MUNGU TU
8.
KUKIRI KUWA MUHAMMAD NI MTUME
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
WA MWENYEZI MUNGU
9.
TWAHARA
10.
SHERIA ZA MWANAWAKE
11.
MWANAMKE KATIKA UISLAMU
12.
SALA
13.
ZAKA
14.
KUFUNGA SAUMU
15.
HIJA NA UMRA
16
.
Huu ni muhtasari wa matendo ya Hija kwa mpangilio:
17
.
FAIDA MBALI MBALI
18.
RUQ-YA KISHERIA
19.
DUA
20.
DUA
MUHIMU
AMBAZO
INATAKIWA
KUZIHIFADHI NA KUOMBA KWAZO
21.
BIASHARA YENYE FAIDA
22.
NYIRADI ZA KILA SIKU, ASUBUHI NA JIONI
23.
KAULI NA VITENDO AMBAVYO NDANI YAKE
KUNA MALIPO MAKUBWA
24.
MAMBO YALIYOKATAZWA
25.
SAFARI YA MILELE
26.
NAMNA YA KUTAWADHA
27.
NAMNA YA KUSALI
28.
ELIMU INAHITAJI UTEKELEZAJI
Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na ubora wake, ukilinganisha na
maneno mengine, ni kama ubora wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake.
Kuisoma Qur'ani ni jambo bora sana ambalo ulimi ume
litamka.
MIONGONI MWA FADHILA ZA KUJIFUNZA QUR'NI NA
KUIFUNDISHA NI:
MALIPO YA KUIFUNDISHA
Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu
amfikishie rehema na amani, amesema kuwa:
"Mbora wenu zaidi ni yule
aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".
Bukhari.
MALIPO YAKUISOMA
Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie
rehema na amani, amesema kuwa:
"Mwenye kusoma herufi katika kitabu cha
Mwenyezi Mungu atapata zuri (moja) kwa herufi hiyo
(moja aliyoisoma), na zuri
(moja) ni kwa mazuri kumi mfano wake
"
.
Tirmidhiy
.
FADHILA ZA KUJIFUNZA QUR’ANI, KUIHIFADHI NA KUISOMA
KWA UHODARI
Amesema Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu
amfikishie rehema na amani, kwamba:
"Mfano wa ambaye anaisoma Qur'ani na
ilhali ni mwenye kuihifadhi, atakuwa pamoja na Malaika, Watukufu, Wema. Na
mfano wa ambaye anaisoma Qur'ani na ilhali yeye anaipatiliza na huku ikiwa
ngumu kwake, basi atapata malipo mawili"
.
Bukhari,
Muslim
.
Na Amesema Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie
rehema na amani, kuwa:
"
Ataambiwa msomaji wa Qur'ani kwamba: Soma na
panda (daraja) na soma kama ulivyokuwa ukisoma duniani, kwani daraja yako ni
pale mwisho wa aya utakayoisoma".
Tirmidhiy
.
MALIPO YA MTU AMBAYE MTOTO WAKE AMEJIFUNZA QUR’ANI
Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema
kuwa:
"Yeyote aliyesoma Qur'ani na akajifunza na akaitekeleza, wazazi wake
watavalishwa taji la nuru Siku ya Kiyama. Mwangaza wake ni mfano wa
mwangaza wa jua. Na wazazi wake watavalishwa suti mbili, na kwa sababu hiyo,
watauliza: Ni kwa sababu ya jambo gani tumevishwa haya? Watajibiwa: Ni kwa
sababu ya mtoto wenu kujifinza Qur'ani"
.
Al-haakim
.
QUR'ANI KUMUOMBEA MSOMAJI WAKE HUKO AKHERA
Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema kuwa:
"Someni Qur'ani, kwani itakuja Siku ya Qiyama ikiwa ni muombezi wa wasomaji
wake"
.
Muslim
.
Aidha Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani,
amesema kuwa:
"Saumu na Qur'ani zitamuombea mja Siku ya Kiyama".
Ahmad, Al-
haakim
.
MALIPO YA KUJUMUIKA KWA AJILI YA KUSOMA QUR'ANI NA
KUIDURUSU
Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na
amani, amesema kuwa:
"Hawakukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa
nyumba za Mwenyezi Mungu Mtukufu wakikisoma kitabu chake na kukidurusu
FADHILA ZA
QUR’ANI
3
baina yao isipokuwa tu unawashukia utulivu na inawaenea rehma na Malaika
huwazunguka na Mwenyezi Mungu huwataja pamoja na viumbe walioko kwake
"
.
Abudaud
BAADHI YA KANUNI ZA USOMAJI:
TARATIBU ZA USOMAJI
Ibn-kathiir ametaja taratibu nyingi. Miongoni
mwake ni hizi: Mtu kutoshika Qur'ani na kutoisoma isipokuwa tu anapokuwa
twahara, kupiga mswaki kabla ya kuisoma Qur'ani, mtu kuvaa nguo zake nzuri
sana, kuelekea Qibla, kusitisha kusoma mtu anapokwenda myayo, kutokatisha
kusoma kwa kuzungumza isipokuwa tu kwa dharura, kuw
a makini, kusitisha
kusoma katika aya za ahadi (za rehma) ili msomaji a
ombe (rehma) na kusitisha
kusoma katika aya za makamio (ya adhabu) ili msomaj
i aombe kinga, kutouweka
msahafu ukiwa umetandazwa chini na kutoweka kitu chochote juu yake, baadhi ya
wasomaji kutosoma kwa sauti ya juu mbele ya baadhi
ya wasomaji wengine (ili
wasiwe kero) katika kusoma na kutosoma masokoni na katika sehemu za zogo.
NAMNA YA KUSOMA
*Kusoma Qur’ani na nyiradi katika sala hakutambuliki mpaka tu mtu atamke
kwa kiasi ajisikilizishe yeye mwenyewe
bila ya kumtatiza mwengine.
*Inatakiwa mtu awe mtulivu katika kusoma kwake. Anas, Mwenyezi Mungu
amuwiye radhi, aliulizwa kuhusu usomaji wa Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi
Mungu amfikishie rehema na amani, akasema:
"(Mtume)
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Alikuwa
anavuta sana anaposoma
"Bismil-laahir-rahmaanir-rahiim
"
Anavuta "
Bismillaah
".
Anavuta
Arrahmaan
Anavuta
"
Arrahiim
"
.
Bukhariy
.
KUSOMA KWA KUHIFADHI
Ikiwa msomaji wa Qurani anapata mazingatio,
tafakuri na umakini zaidi akisoma kutokana na kuhifadhi kwake, basi
kusoma kwa
kuhifadhi ni bora zaidi
kuliko kuangalia msahafu. Ikiwa kusoma kwa kuhifadhi
na kuangalia msahafu kuko sawa,
basi kusoma kwa kuangalia msahafu ni bora
zaidi
.
USIA
:
Ndugu yangu, fanya bidii ya kuutumia wakati wako katika kuisoma
Qur'ani
. Jiwekee
kiwango cha kila siku
na usikiache vyovyote iwavyo. Kichache
kinachodumu ni bora zaidi kuliko kingi kisichodumu. Ikiwa utaghafilika au utalala,
basi kilipe kesho. Mtume,
(
Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam
)
Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na
amani, amesema kuwa:
"
Aliyelala akapitwa na hizbu (uradi) yake au sehemu
ya
hizbu yake akaisoma katika wakati uliopo baina ya sala ya Alfajiri na sala ya
Adhuhuri, ataandikiwa kama ameisoma usiku"
.
Muslim
.
Usiwe miongoni mwa walioiacha Qur'ani au kuisahau
kwa namna yoyote;
kama kuacha kuisoma au kuacha kuizingatia au kuacha kuitekeleza au kuacha
kuifanya tiba.
TAFSIRI YA SHEMU YA KUMI YA MWISHO YA QUR’ANI TUKUFU
سنة النشر : 2011م / 1432هـ .
حجم الكتاب عند التحميل : 21.5 ميجا بايت .
نوع الكتاب : pdf.
عداد القراءة:
اذا اعجبك الكتاب فضلاً اضغط على أعجبني و يمكنك تحميله من هنا:
شكرًا لمساهمتكم
شكراً لمساهمتكم معنا في الإرتقاء بمستوى المكتبة ، يمكنكم االتبليغ عن اخطاء او سوء اختيار للكتب وتصنيفها ومحتواها ، أو كتاب يُمنع نشره ، او محمي بحقوق طبع ونشر ، فضلاً قم بالتبليغ عن الكتاب المُخالف:
قبل تحميل الكتاب ..
يجب ان يتوفر لديكم برنامج تشغيل وقراءة ملفات pdf
يمكن تحميلة من هنا 'http://get.adobe.com/reader/'